CHELSEA YAMTUPILIA MBALI DIEGO COSTA,SOMA ZAIDI HAPA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Saturday, January 14

CHELSEA YAMTUPILIA MBALI DIEGO COSTA,SOMA ZAIDI HAPA

 Image result for diego costa
STRAIKA Diego Costa ametupwa nje ya Kikosi cha Chelsea ambacho Leo kipo huko King Power Stadium kucheza na Mabingwa Watetezi Leicester City katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.

 
Habari za ndani zimedai upo mzozo wa Costa, mwenye Miaka 28, na uongozi wa Klabu akisindikiza ahamie China kwa Dau la Pauni Milioni 30.

Hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la Wachezaji Wakubwa Duniani kutua huko China ambako wanalipwa Mishahara minono mno.

Wiki yote hii, Costa amekuwa hayupo Mazoezini akidai ameumia na pia kuzozana na Madktari wa Viungo wa Chelsea mzozo ambao umesekana ulimhusisha pia Meneja Antonio Conte.

Hivi sasa ripoti zimedai Wakala wa Conte, Jorge Mendes, yupo huko China.

Kikosi cha Chelsea ambacho Jana kilijumuika pamoja kuelekea huko Leicester kiliondoka bila Costa.

Hata hivyo, msimamo wa Chelsea ni kwamba hawatamuuza Mchezaji huyo Mzaliwa wa Brazil anaechezea Spain na watabaki nae hadi mwisho wa Mkataba wake hapo 2019.

Msimu huu, Costa ameifungia Chelsea Bao 14 na kuasisti mara 5 huku Chelsea ikiongoza EPL ikiwa Pointi 5 juu kileleni mbele ya Timu ya Pili Liverpool.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here