Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es Salaam (ARU) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kupandishwa kizimbani akikabiliwa na kosa la kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa What’sApp.
Akimsomea
hati ya mashtaka, mshtakiwa huyo, Wakili wa Serikali, Adolf Mkini mbele
ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa alidai kuwa mshtakiwa huyo
ambaye pia anadaiwa kuwa ni kada wa Chadema Januari 3, 2017
alichapisha taarifa za uongo.
Alidai
kuwa mshtakiwa huyo kupitia mtandao wa WhatsApp kwenye kundi
linalotumia jina la Lowassa Foundation and Bunge Live alichapisha
taarifa za uongo kuwa; Nimepata rehema ya mipango michafu sana iliyokuwa inapangwa na bado inapangwa dhidi ya uhai wa (Mb), Godbless Lema…’
Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana kuhusika na kosa hilo.
Upande wa mashtaka umedai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na hana pingamizi na dhamana.
a
Baada
ya kueleza hayo, Hakimu Mwambapa alimpa masharti ya dhamana mshtakiwa
huyo ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh 2 milioni kwa
kila mmoja pamoja na barua.
Hata hivyo, mshtakiwa huyo aliepuka kwenda lumande baada ya kutimiza masharti hayo ya dhamana.
No comments:
Post a Comment