TUZO ZA CAF KESHO ZITATOLEWA RASMI,HABARI ZOTE HAPA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Wednesday, January 4

TUZO ZA CAF KESHO ZITATOLEWA RASMI,HABARI ZOTE HAPA

SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF kesho linatarajia kufanya sherehe ya kutoa tuzo kwa wachezaji mbalimbali wa soka waliofanya vizuri katika kipindi cha mwaka mzima uliopita.

Sherehe hizo zinakuwa ni za 25 toka kuanzishwa kwake na zinatarajiwa kufanyika jijini Abuja, Nigeria kwa mara ya pili mfululizo.


Kwenye sherehe hizo atapatikana mfalme wa soka Afrika ambapo miongoni mwao ni pamoja na mshindi wa tuzo ya mwaka jana Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon, Riyad Mahrez wa Algeria na Sadio Mane anayetoka Senegal.

Kuanzia mwaka 1992 zilipoanzishwa tuzo hizo ambapo ilikwenda kwa nguli wa zamani wa Ghana Abeid Ayew Pele mpaka mwaka jana alipotwaa Aubameyang ni jumla ya wachezaji 15 waliofanikiwa kutwaa hiyo.

Nyota wa Cameroon Samuel Eto’o ndio mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo hiyo mara nne mfululizo mwaka 2003, 2004, 2005 na 2010 kabla ya Yaya Toure wa Ivory Coast hajaivunja rekodi hiyo kwa kutwaa kuanzia mwaka 2011 mpaka 2014.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here