Mgogoro wa Uongozi wa Chama cha
Wananchi CUF umeendelea kufukuta ambapo Mwenyekiti wa Chama hicho
anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili Vyama vya Siasa nchini Prof. Ibrahim Lipumba
amemteua Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya kukaimu nafasi ya Katibu Mkuu
Maalim Seif Sharif Hamad baada ya Maalim Seif kukaidi wito wa Mwenyekiti wake
kwenda Ofisi kuu Buguruni kwa zaidi ya mara nne
Prof. Lipumba akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam pamoja na wafuasi wa chama hicho,
amesema Maalim Seif amekaidi wito wa kwenda Makao Makuu ya chama hicho zilizopo
Buguruni tangu Septemba 23 mwaka jana kwa ajili ya kusimamia mkutano wa kamati
ya Utendaji ambao ulitakiwa kujadili mambo kadhaa ya chama hicho
Aidha, Prof. Lipumba amewavua
madaraka wakurugenzi kutoka Zanzibar akiwemo Salim Bimani aliyekuwa Mkurugenzi
wa Habari na Uenezi, Omar Ali Salehe Mkurugenzi Mipango na Uchaguzi, Abdalah
Bakar Khamis Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi, Pavu Juma Abdallah - Haki za
Binadamu, Mahima Ali Mahima Katibu Mtendaji JUVICUF pamoja na Yusuph Salim
Naibu Mkurugenzi Ulinzi na Usalama CUF wote kutoka Zanzibar.
Chama cha Wananchi CUF kimekumbwa na
Mgogoro wa uongozi tangu Prof. Lipumba alipotangaza kujiuzulu uongozi wa chama
hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, ambapo baadaye alitangaza kurudi na
kufanyika mkutano mkuu ambao ulivurugika na kusababisha mpasuko kati ya CUF
bara na CUF Zanzibar.
No comments:
Post a Comment