Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe
13 Machi 2017, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein
Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma.
Dkt.
Magufuli amesema katika mazungumzo yao wamezungumza mambo mbalimbali
ikiwa ni pamoja na kumtakia heri Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kufuatia leo kuwa siku yake
ya kuzaliwa.
Kwa
upande wake Rais Dkt. Ali Mohamed Shein amesema anamshukuru Rais
Dkt.Magufuli kwa kumtakia heri katika siku yake muhimu ya kuzaliwa na
hivyo wamekutana kubadilishana mawazo katika kuhakikisha wanajenga nchi
na kusonga mbele.
''Siku
ya kuzaliwa ni siku ya furaha lazima ikumbukwe lazima isherehekewe,
mimi siku yangu ya kuzaliwa sisherehekei sana lakini huwa nafurahi sana
na leo nimefurahi sana'' amesema Dkt. Shein.
Dkt.Shein
amesema ametumia siku yake ya kuzaliwa kumtembelea Rais Dkt.Magufuli
ili waweze kubadulishana mawazo kwani wana kazi kubwa ya kujenga nchi.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dodoma
No comments:
Post a Comment