Afrika Kusini yaadhimisha miaka 41 ya mauaji ya wanafunzi weusi Soweto - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Saturday, June 17

Afrika Kusini yaadhimisha miaka 41 ya mauaji ya wanafunzi weusi Soweto


Raia nchini Afrika Kusini waadhimisha miaka 41 tangu mauaji ya wanafunzi weusi na polisi weupe wa ubaguzi wa rangi.

Wanafunzi weusi walikuwa wanaandamana katika kitongoji cha Soweto jijini Johannesburg mnamo mwaka 1976 kupinga lugha ya Afrikaans kutumika kama lugha rasmi katika shule .

Kipindi hicho serikali ilikuwa chini ya watu weupe,polisi waliwaua wanafunzi hao waliokuwa wanaandamana kwa risasi .

Wanafunzi wengi waliuawa na idadi kamili ya waliouawa haijulikani .

Hafla mbali mbali kote nchini zimeandaliwa na serikali na upinzani ishara ya heshima kwa wanafunzi waliojitoa mhanga kipindi hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here