Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 48 amekamatwa kufuati kisa hicho huku polisi wa kupambana na ugaidi katika eneo hilo wakielielezea tukio hilo kama la kigaidi.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May amekitaja kuwa kisa kibaya akisema kuwa fikra zake ziko kwa wale waliojeruhiwa, wapendwa wao na watoa huduma za dharura eneo hilo.
Idara ya kutoa huduma za dharura Jijini London imesema imetuma huduma kadha eneo hilo.
Video iliyowekwea katika mitandao ya kijamii ilionyesha vurugu huku watu wakiwasaidia wale waliojeruhiwa.
Baraza Kuu la Waislamu nchini Uingereza limesema kuwa walengwa wa tukio hilo walikuwa ni waumini, huku majeruhi wengi wakiaminika kuwa ni wale waliokuwa wamemaliza tu kuswali swala ya jioni baada ya kuumaliza mfungo wa siku wa Ramadhani.
No comments:
Post a Comment