Mitambo ya kughushi nyaraka yakamatwa na Uamiaji - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Friday, June 16

Mitambo ya kughushi nyaraka yakamatwa na Uamiaji


Kamishna wa Usimamizi wa Mipaka, Samwel  Magweiga

IDARA ya Uhamiaji imekamata mitambo ya kughushi nyaraka mbalimbali za idara hiyo pamoja na mashine za kielektroniki (EFDs).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Usimamizi wa Mipaka, Samwel Magweiga alisema nyaraka hizo zilikuwa zikimilikiwa kinyume cha sheria na kuikosesha serikali mapato stahiki.


“Tumewakamata watu watano ambao walikuwa wakijifanya ni mawakala wa idara yetu na walikuwa wakiwatapeli wananchi kwa kujifanya ni maofisa wa idara ya uhamiaji wakati ni mapateli.

“Mpaka sasa upelelezi umekamilika na kwamba wakati wowote tutawafikisha mahakamani ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria,” alisema Magweiga.

Alisema watu hao wamekuwa wakitumia mitambo mbalimbali ya kughushi zinazofanywa na idara hiyo huku wakijua kuwa wanachokifanya ni kinyume cha sheria.

Licha ya mitambo hiyo, watu hao wamekutwa na nyaraka zinazoonyesha shughuli za serikali zikiwamo miradi ya maendeleo pamoja na mashine za kielektroniki (EFDs) zinazotumika kukusanya fedha za Serikali.

Kutokana na hali hiyo, idara hiyo imepiga marufuku watu wote wanaojifanya mawakala wa idara hiyo na kufanya kazi zinazofanana na uhamiaji kinyume cha sheria na kuonya kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria ikiwamo kufikishwa mahakamani.

Alisema, wananchi wanaotaka huduma kutoka idara hiyo wanapaswa kufika kwenye ofisi za uhamiaji popote zilizopo ili waweze kuhudumiwa kwa mujibu wa sheria.

Aliongeza kwamba ili kuepusha utapeli huo, wananchi wanapaswa kushirikiana na idara hiyo kwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika juu ya watu wanaojifanya mawakala ili waweze kutafutwa na kuchukuliwa hatua za kisheria, jambo ambalo linaweza kupunguza ukubwa wa tatizo.

Alisema mpaka sasa idara hiyo imepata taarifa ya kuwepo kwa magenge ya wahalifu wanaotumia jina la idara hiyo kwa ajili ya kuwatapeli wananchi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here