Mjane wa Mtikila ateuliwa kuwa mwenyekiti wa DP - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Tuesday, June 20

Mjane wa Mtikila ateuliwa kuwa mwenyekiti wa DP







Chama cha Democratic Party(DP) kimemteua Georgia Mtikila kuwa mwenyekiti wa chama hicho kitaifa kwa kipindi cha miaka mitano kwa mujibu wa katiba.

Georgia alikaimu nafasi hiyo tangu alipofariki dunia mwasisi wa DP, Christopher Mtikila kwa ajali ya gari Oktoba 2015 maeneo ya Chalinze Mkoa wa Pwani.

Katika taarifa iliyotumwa katika vyombo vya habari leo Juni 20, Georgia amewataka wajumbe wa chama hicho mikoani kufanya kazi kwa kufungua matawi ili kukiimarisha chama hicho katika ngazi zote.

“Mkaimairishe chama kwa kufungua matawi katika ngazi zote za mkoa, wilaya, kata, tawi, kitongoji na shina ili kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji 2019 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020,” amesema Georgia katika taarifa hiyo.

Georgia ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu, amewataka viongozi wa chama hicho waliochaguliwa kuwa na mshikamano wa pamoja wa kukijenga chama na kuachana na majungu na masengenyo.

Amewasihi viongozi hao kusoma katiba na kuielewa ili kusaidia katika shughuli zao, kujiepusha na migogoro ya chama.

Alisema migogoro ikitokea wanatakiwa kufuata katiba ya chama au itakapozidi wahusika wakatafute suluhu nje ya chama.

Georgia amewataka viongozi wa Serikali hasa ofisi ya Msajili kuheshimu yaliyomo ndani ya katiba za vyama vya siasa na kama kuna mapungufu ya vipengele awape ushauri.

“Ofisi ya msajili inatakiwa kuheshimu yaliyomo katika baadhi ya vipengele ndani ya katiba zao, kama kuna kasoro basi msajili anaweza kushauri kuvibadili au kuvifuta vipengele husika,” amesema Georgia.


Viongozi wengine 19 waliochaguliwa katika mkutano wa chama  ni pamoja na Dastan Malle ambaye amekuwa Makamu Mwenyekiti na Haji Ally Makamu ambaye ni Mwenyekiti wa DP Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here