Mwanasiasa huyo alishinda kwa kura 57 dhidi ya 50 baada ya wabunge kupiga kura, na kumfanya kuwa kiongozi mchanga zaidi wa nchi hiyo na pia kiongozi wake wa kwanza mpenzi wa jinsia moja.
Wabunge 47 walisusia kura hiyo.
Varadkar ni mwana wa mwuguzi mzaliwa wa Ireland na daktari kutoka India.
Alijishindia uongozi wa chama cha Fine Gael mwezi uliopita.
Amemteua aliyekuwa anashindana naye kuongoza chama hicho Simon Coveney kuwa naibu wake.
Akihutubu katika bunge la Ireland, Dáil, baada ya kuchaguliwa, Bw Varadkar amesema: "Nimechaguliwa kuongoza na naahidi kuwatumikia wananchi."
"Serikali ninayoiongoza si ya mrengo wa kushoto au kulia kwa sababu migawanyiko hiyo ya zamani haina ufahamu kuhusu siasa za siku hizi.
Bw Varadkar baadaye ameelekea makao ya rais, Áras an Uachtaráin, ambapo Rais Michael D Higgins amempa vifaa vya uongozi kuthibitisha kuteuliwa kwake.
Miongoni mwa watu wa kwanza kumpongeza ni Rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker, ambaye amesisitiza kuhusu changamoto inayotolewa na hatua ya Uingereza kuamua kujiondoa kutoka kwa Umoja wa Ulaya.
Varadkar alichaguliwa diwani akiwa na miaka 24 na akawa mbunge mwaka 2007.
No comments:
Post a Comment