Mtanzania Miezi Mitatu Jela Uingereza kwa Kupost picha ya Maiti, Facebook - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Saturday, June 17

Mtanzania Miezi Mitatu Jela Uingereza kwa Kupost picha ya Maiti, Facebook




MTU mmoja anayetambulika kwa jina la Omega Mwaikambo anayedaiwa kuwa ni Mtanzania amehukumiwa miezi mitatu jela kwa kosa la  kupiga picha ya mwili wa mtu aliyefariki uliokuwemo kwenye mfuko maalum wa kuhifadia maitiuziweka kwenye facebook.

Maiti hiyo inayodaiwa aliyedaiwainayodhaniwa kuwa ilitokana na ajali ya moto katika jengo la Grenfell Tower iliyotokea hivi karibuni jijini London huko nchini Uingereza.

Mtuhumiwa huyo alipandishwa kizimbani jana Juni 16, 2017 katika Mahakama ya Hakimu Westminster na kusomewa mashtaka yake na kuhukumiwa kwenda jela kwa miazi mitatu kwa kutenda kosa hilo.



Mtuhumiwa huyo ambaye anaishi eneo la jirani kabisa na jengo la Grenfell Tower lililopatwa na janga la kuteketea kwa moto.



Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo, alifanya hivyo siku ya jumatano asubuhi, alipotoka nje ya nyumba yake na kukuta mfuko huo wenye mwili na kuufungua kisha kuupiga picha na kurekodi video alizoziweka kwenye mtandao wa Facebook huku akiuliza "Je, kuna mtu yeyote anaujua mwili huu ambao uko nje ya ghorofa langu kwa zaidi ya saa mbili?"

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here