Radio sauti ya Qur,an yafanya maadhimisho ya kihistoria - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Friday, June 16

Radio sauti ya Qur,an yafanya maadhimisho ya kihistoria



Maelfu ya waumini kote nchini wamejitokeza katika maadhimksho ya mkesha wa lailatul kadir  kama yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha kiisalamu cha Alharamain jijini Dar es salaam.

Maadhimisho hayo yaliyofunguliwa rasmi kwa dua na muhadhir wa kiislamu nchini sheikh chizenga nakisha kuendelea na visimamo vya swala ya tarawekh na visimamo vya usiku.

Akiongea katika maadhimisho hayo sheikh chizenga aliwahimiza waumini wa dini hiyo kujikurubisha zaidi na Mola wao na kuomba msamaha kwa wongi hasa katika mwezi huu mtukufu wa ramadhani.

Naye mtangazaji wa Radio sauti ya Qur'an bwana Jamil Poli alitumia fursa hiyo kuwashukuru wote waliofika na kuwaomba waumini kujitokeza kwa wingi mwakani ili kuonesha umoja na mshikamano miongoni mwa waislamu na kuwaomba ushirikiano katika jambo lolote la dini.

Maadhimisho hayo ambayo huandaliwa kila mwaka na Radio sauti ya Quran hulenga kuwakusanya pamoja waumini ya dini ya hiyo ili kuutafuta usiku uliobora zaidi (Lailatul Qadir) ambao hupatikana katika kumi la mwisho lamwezi wa mtukufu wa Ramadhan.

Radio sauti ya Qur'an ndiocho  kikongwe zaidi nchini  katika vituo vya dini ya kiislamu kikiwa na zaidi ya miaka 20.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here