Taarifa hiyo imearifiwa na shirika la masuala ya uhamiaji (IOM) mapema siku ya Jumanne .
Wakati huo huo msemaji wa IOM alifahamisha kwamba wahamiaji wanne waliweza kuokolewa .
Wengi wa wahamiaji hao ni raia wa Nigeria na Sudan .
Shirika la uhamiaji la UN lafahamisha kwamba takriban wahamiaji 44,209 wameingia Ulaya mwaka 2017 ,wengi wao wameenda Italia ,Ugiriki,Uhispania na Cyprus .
Wahamiaji wasiopungua 966 wamezama na kupotea katika bahari ya Mediterania katika njia inayounganisha Afrika kaskazini na Italia .
No comments:
Post a Comment