Wanaume 1,500 wilayani Bariadi mkoani Simiyu kufanyiwa tohara. - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Sunday, June 18

Wanaume 1,500 wilayani Bariadi mkoani Simiyu kufanyiwa tohara.


Zaidi ya wanaume 1,500 wilayani Bariadi mkoani Simiyu wanatarajia kufanyiwa tohara ili kujikinga na maambukizi ya magonjwa mbalimbali kwa asilimia 60.

Hatua hiyo imetokana zoezi lilofanywa na madaktari bingwa kutoka katika Tasasi ya Kiislamu ya The Islamic Foundation kwa ushirikiano na kampuni ya ununuzi wa zao la pamba Alliance Ginnery linalofanyika katika kijiji cha Kasoli na vijiji jirani wilayani humo.

Wakizingumza katika zoezi hilo la upimaji afya na kupatiwa matibabu bure wananchi hao wanaeleza kuwa hatua hiyo ni nzuri kwao,kwani wengi wao wamekuwa wakishindwa kumudu gharama za matibabu katika vituo vya afya na kusababisha kukosa huduma za afya wanazozihitaji.

Mratibu wa mpango afya salama na mtoto wilayani Bariadi,Pamela Charles amesema sehemu zote ambazo wanaume hawajafanyiwa tohara lipo tatizo kubwa kwa akina mama walioolewa kupata tatizo la shingo ya kizazi na kwamba ujio wa huduma hiyo utasaidia kupunguza tatizo hilo ambapo ametoa wito kwa wanaume wajitokeze kwa wingi.

Kaimu Mkurugenzi wa Islamic Foundation,mbaraka saidi amesema lengo la kutoa huduma hiyo ni kuwafikishia huduma ambazo wengi wamekuwa hawazipati kwa muda muafaka hali ambayo imekuwa ikiwalazimu kutembea umbali mrefu.
Mbali na  kutoa huduma ya tohara pia madktari hao wamefanya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi,tezi dume  na magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa miwani bure kwa wagonjwa wa macho.

1 comment:

Post Top Ad

Responsive Ads Here