Kenya yaipiga bao Tanzania - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Wednesday, October 4

Kenya yaipiga bao Tanzania


Wanariadha wawili wa Kenya wametajwa kuwania tuzo za riadha za dunia kwa mwaka 2017 na kuifanya nchi hiyo kuwa taifa pekee kutoka Afrika Mashariki kuingiza wanariadha katika tuzo hizo.

Elijah Manangoi ni mwanariadha pekee kutoka Kenya ambaye ametajwa kwenye orodha ya wanariadha 10 wa kiume na Hellen Obiri ambaye yumo katika orodha ya wanariadha kumi wa kike wanaowania tuzo hiyo.

Mbali na wakenya hao, pia yumo Muethiopia mmoja ambaye ni Almaz Ayana pamoja na wanariadha watatu kutoka Afrika Kusini akiwemo Caster Semenya.
Orodha kamili ya wanariadha wanaowania tuzo za dunia ni:-
Wanaume:
Mutaz Essa Barshim (Qatar); Pawel Fajdek (Poland); Mo Farah (Uingereza); Sam Kendricks (Marekani); Elijah Manangoi (Kenya); Luvo Manyonga (Afrika Kusini); Omar McLeod (Jamaica); Christian Taylor (Marekani); Wayde van Niekerk (Afrika Kusini); Johannes Vetter (Ugiriki).

Wanawake:
Almaz Ayana (Ethiopia); Maria Lasitskene (Urusi); Hellen Obiri (Kenya); Sally Pearson (Australia); Sandra Perkovic (Croatia); Brittney Reese (Marekani); Caster Semenya (Afrika Kusini); Ekaterini Stefanidi (Ugiriki); Nafissatou Thiam (Ubelgiji); Anita Wlodarczyk (Poland).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here