Bobi Wine.
Taarifa zinasema kwamba nyumba za wabunge hao wawili ni pamoja na Mwanamuziki Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) ambaye amesema kwamba shambulio hilo lilikuwa likimlenga yeye kwa kile alichosema kupingana na chama tawala ambacho kinataka kubadilisha katiba na kutokuwa na kikomo cha umri wa kuwania urais wa nchi hiyo.
Aidha Mbunge Bobi Wine amesema amekuwa akipokea vitisho vya kuawa takribani kila siku kwa sababu ya kupinga kwake katika mjadala unaoendelea wa kuondoa kikomo cha umri katika kuwania urais nchini Uganda.
Hata hivyo Polisi sasa wanachunguza mashambulizi kwenye nyumba za Mbunge Bobi Wine ambaye anayewakilisha eneo la Kyaddondo West na Allan Ssewanya ambaye ni mbunge wa Makindye West.
Gazeti la New Vision limedai kuwa wabunge ambao nyumba zao zilishambuliwa ni badhi ya wale waliotimuliwa bungeni kufuatia ghasia wakati wa mijadala kuhusu kuondolewa kwa umri wa kuwania urais.
Bobi Wine amethibitisha kwa kusema kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa nyumbani kwake hata baada ya shambulio hilo.
Wabunge Kyagulanyi na Allan Ssewanyana wamesema nyumba zao zilitetemeshwa na mlipuko huo na madirisha kuvunjika kutokana na mlipuko huo. Msemaji wa serikali amekanusha serikali kuhusika na shambulio hilo.
No comments:
Post a Comment