Amuua mume wake kisa wivu wa mapenzi - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, November 9

Amuua mume wake kisa wivu wa mapenzi


MASUMBUKO Stephano mkazi wa Mtaa wa Kamando, Kata ya Igunga Mjini, Igunga mkoani Tabora, amefariki dunia papo hapo baada ya kuchomwa kisu na mkewe Christina  Elias (30) kutokana na kile kinachosadikiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Julius Kitundu alisema Stephano (39) alifariki dunia katika tukio hilo lilitokea juzi saa 7:15 usiku.

Alisema siku ya tukio, mke wa Stephano baada ya kugundua kwamba mumewe yuko kwa mpenzi wake, Happiness Wiliam (28), aliamua kumfuata huko na baada ya kufika aligonga mlango na kisha kuingia ndani ya chumba walichokuwapo wapenzi hao wawili.

Kwa mujibu wa mwenyekiti  huyo, baada ya Christina kuingia ndani ya chumba walichokuwamo, alimchoma mumewe kisu upande wa kushoto katika eneo la moyo na ndipo mumewe alianguka chini na kupoteza maisha.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Dk. Habilo Mhagama, alikiri kupokea mwili wa Masumbuko Stephano majira ya saa nane usiku na kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha marehemu alipoteza maisha baada ya kuvuja damu nyingi kutokana na kisu alichochomwa kwenye moyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here