Baada
ya kusaini mkataba wa miaka miwili, beki wa pembeni wa Simba, Mohamed Zimbwe
maarufu kama 'Tshabalala', ametamka kuwa haidai timu hiyo lakini yenyewe ndiyo
inamdai deni kubwa la kuhakikisha anaipa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.
Tshabalala
alisaini mkataba huo wiki iliyopita baada ya ule wa kwanza kubakiza miezi sita.
Beki
huyo anayecheza namba tatu, kabla ya kusaini mkataba huo alikuwa akiwaniwa
vikali na Yanga ambayo ilitenga kitita cha Sh mil 60 ili kumnasa. Hata hivyo,
Simba inafanya siri kuhusu dau ililompa ili amwage wino.
Tshabalala
alisema amepanga kuitumikia timu hiyo kwa mafanikio makubwa katika kipindi
chote atakachokuwepo Simba.
Tshabalala
alisema, moja ya mafanikio atakayoanza nayo ni kuuchukua ubingwa wa Ligi Kuu
Bara nchini ya Kocha Mkuu Mcameroon, Joseph Omog.
Aliongeza
kuwa, Wanasimba watarajie mengi kutoka kwake, hiyo ni baada ya kumalizana na
viongozi wake kwa kutimiza mahitaji yake muhimu aliyokuwa anayahitaji ikiwemo
fedha ya usajili na mshahara mzuri, hivyo ni lazima afanye kazi katika kiwango
cha juu ili kuipa mafanikio timu hiyo kwa kuwa sasa akili yake imetulia.
“Mimi
Simba siwadai, wao ndiyo wananidai, hivyo ni lazima nifanye kazi yangu vizuri
katika kuhakikisha ninaipa mafanikio makubwa timu yangu ya Simba.
"Mafanikio
hayo ni kuipa mataji mbalimbali ya ubingwa kwa kuanzia huu wa ligi kuu, hivyo
ninaahidi kupambana ndani ya uwanja kuhakisha ninafikia malengo yangu.
“Na
hilo litawezekana kama wachezaji, viongozi na benchi la ufundi tutaungana na
kufanya kazi kwa pamoja kwa kushirikiana kwa kila mmoja kutimiza majukumu
yake,” alisema Tshabalala.
No comments:
Post a Comment