JOSE MOURINHO ATOLEWA NJE MAN U IKITOA SULUHU,ANGALIA NA RATIBA YA WIKI IJAYO - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Sunday, November 27

JOSE MOURINHO ATOLEWA NJE MAN U IKITOA SULUHU,ANGALIA NA RATIBA YA WIKI IJAYO

                  Image result for MANCHESTER UNITED

MANCHESTER UNITED wametoka Sare yao ya 4 mfululizo ya EPL, Ligi Kuu England, Uwanjani kwao Old Trafford walipotoka 1-1 na West Ham.
 
Sekunde 90 tu tangu Mechi ianze, West Ham walifunga Bao kwa Frikiki ya Dimitri Payet kuunganishwa na Diafra Sakho na kuwapa Bao.

Man United walitulia na kukontroli Gemu na kusawazisha Bao Dakika ya 21 kufuatia muvu ya Pasi 22 ikiguswa na kila Mchezaji wa Man United na kisha kumfikia Paul Pogba na kummiminia Zlatan Ibrahimovic aliefunga kwa Kichwa.

Mabao hayo yalidumu hadi Haftaimu lakini matukio makubwa katika Kipindi cha Kwanza hicho ni Paul Pogba kupewa Kadi ya Njano na Refa Jon Moss kwa madai ya kujiangusha na Kadi hiyo kumfanya Pogba sasa apate Kifungo cha Mechi 1 kwa kuwa amezoa Kadi za Njano 5 na ataikosa Mechi ifuatayo Jumatano ya EFL CUP dhidi ya hao hao West Ham Uwanjani Old Trafford.

Tukio hilo lilimkasirisha sana Jose Mourinho na kuibutua Chupa ya Maji kwenye Eneo lake la Ufundi na Refa Moss kumtoa Uwanjani aende Jukwaani kwa Watazamaji akimwacha Msaidizi wake Lui Faria kukaimu.

Mechi inayofuata ya EPL kwa Man United ni Ugeni huko Goodison Park dhidi ya Everton ambao Leo walichapwa 1-0 huko Saint Mary kwa Bao la Sekunde ya 43 tu la Charlie Austin walipocheza na Southampton.

Ratiba:
**Saa za Bongo
Jumamosi Desemba 3
1530 Manchester City v Chelsea      
1800 Crystal Palace v Southampton          
1800 Stoke City v Burnley              
1800 Sunderland v Leicester City              
1800 Tottenham Hotspur v Swansea City             
1800 West Bromwich Albion v Watford                
2030 West Ham United v Arsenal              
Jumapili Desemba 4
1630 Bournemouth v Liverpool                
1900 Everton v Manchester United            
Jumatatu Desemba 5
2300 Middlesbrough v Hull City       

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here