Mechi za Robo Fainali ya EFL CUP, Kombe la Ligi la England, zinaanza Leo hii kwa Mechi mbili kwenye Viwanja Viwili tofauti.
Huko Anfield Liverpoool watacheza na Timu ya Daraja la chini Leeds United wakati huko Kingston Communications Stadium ni Hull City na Timu ya Daraja la chini la Championship Newcastle United.
Liverpool wataingia kwenye Mechi hii wakiwakosa Nyota wao kadhaa ambao ni Majeruhi na ambao ni Phlippe Coutinho, Daniel Sturridge na Adam Lallana.
Hata hivyo Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amethibitisha mbali ya Golini kumweka Kipa Simon Mignolet badala ya Nambari Wake Loris Karius hatafanya mabadiliko yeyote kwani amekiri Leeds ni tishio.
Leeds, chini ya Meneja Garry Monk, wapo Nafasi ya 5 kwenye Championship na Timu ambayo kwenye Miaka ya nyuma ilitikisa Vigogo wa England.
Jumatano pia zipo Mechi 2 za Robo Fainali na zote ni za Timu za EPL pekee ambako huko Emirates ni Arsenal na Southampton na huko Old Trafford ni Manchester United na West Ham United.
EFL CUP
Robo Fainali
Ratiba
Jumanne Novemba 29
22:45 Hull City v Newcastle United
22:45 Liverpool v Leeds United
Jumatano Novemba 30
22:45 Arsenal v Southampton
23:00 Manchester United v West Ham United:
No comments:
Post a Comment