KOCHA wa Brazil Tite amesema Kikosi chake kinakaribia kuwa na hakika na kufuzu kwa safari ya kwenda Russia kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018.
Tangu atwae wadhifa kutoka kwa Dunga Mwezi Juni, Tite aliitoa
Brazil kutoka Nafasi ya 6 ya Kundi la Nchi 10 za Kanda ya Marekani ya
Kusini kwa kushinda Mechi zao zote 6 wakifunga Bao 17 na kufungwa 1 tu
na kukamata Nafasi ya Kwanza ya Kundi hilo wakiwa na Pointi 27 kwa Mechi
12.
Nchi 4 za juu za Kundi hilo lenye Nchi 10 zitafuzu moja kwa moja
kwenda Russia na ya 5 kutinga Mechi ya Mchujo ili kusaka nafasi ya
kufuzu.
Akiongea hapo Jana kwenye Mahojiano maalum, Tite alisema
ameshangazwa na Timu kubadilika kutoka lile janga la kubandikwa 7-1
kwenye Nusu Fainali ya Kombe la Dunia na Germany kwenye Mechi
iliyochezwa Nchini kwao Mwaka 2014.
Tite amesema: "Tunajenga msukumo mpya kwa Timu ya Taifa. Tunaijenga Timu ili tufuzu kwa kucheza Soka safi lenye tija."
Mwezi Machi Brazil wataenda Ugenini kucheza na Uruguay na ushindi
huko utawaweka karibu ya kufuzu na kudumisha ile rekodi yao ya kuwa Nchi
pekee Duniani iliyocheza kila Fainali ya Kombe la Dunia.
Kabla ya Tite kutua Brazil, Timu hiyo maarufu kwa wenyewe kama
Selecao, ililaumiwa sana kwa kumtegemea mno Neymar lakini sasa mbali ya
Fowadi huyo wa Barcelona wapo Vijana wengine wanaoibeba vizuri mno
wakiwamo Philippe Coutinho na Gabriel Jesus.
No comments:
Post a Comment