POLISI NCHINI UGANDA WAKABILIANA NA WAPIGANAJI WA MFALME - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Sunday, November 27

POLISI NCHINI UGANDA WAKABILIANA NA WAPIGANAJI WA MFALME

Na Mustafa Ismail

Takriban watu 14 wameuawa nchini Uganda ,katika makabiliano kati ya maafisa wa polisi na wapiganaji wanaohusishwa na mfalme mmoja wa kitamaduni nchini humo.


ramani ya uganda
Wapiganaji hao wanadaiwa kushambulia kituo kimoja cha polisi katika mji wa Magharibi wa Kasese ,ambao ndio nyumbani kwa mfamle wa Rwanzururu Charles Wesley Mumbere.
Wapiganaji wanane pamoja na maafisa 2 wa polisi walifariki.
Msemaji wa serikali ya Uganda iliwashtumu wapiganaji kwa kutaka kujitenga na Uganda.
''Hawa wapiganaji wameanzisha kambi katika milima ya Rwenzori ambapo hujipatia mafunzo na kuja kujaribu kushambulia taasisi za serikali'',alisema Shaban Bantariza.
Mfalme huyo amekana madai ya kuhusishwa na wapiganaji hao.
Jamii yake ya Bakonzo iliopo mpakani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekuwa ikikabiliana kwa muda mrefu na jamii ya ufalme wa Tori katika eneo hilo.
Miaka kadhaa ya mapigano ilikamilika 1982 kukiwa na makubaliano ya kuwepo na uhuru huku rais Museveni akitambua rasmi ufalme huo 2009, lakini wasiwasi umezidi kutanda.
Kati ya mwezi Februari na Machi mwaka huu, zaidi ya watu 50 waliuawa katika ghasia kati ya vikosi vya usalama na waasi kulingana na takwimu za polisi.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here