Na Mustafa Ismail
Wakazi wa wilaya ya
temeke mtaa wa sambwisi wamelalamikia miundombinu mibaya ya barabara katika makutano ya barabara ya sambwisi na
chihota ambapo maji hutulia katika barabara hizo kero ambayo wameitaja
kurudisha nyuma maendeleo kwani hukwamisha shughuli za uchukuzi na biashara
pindi mvua inaponyesha.
Akiongea na Mkwelitz mapema wiki hii mmoja wa wakaazi wa eneo
hilo na mfanya biashara Musa Ali ameelekeza kidole cha lawama kwa serikali ya
wilaya hiyo na kusema kuwa serikali hiyo inakwepa majukumu “Mimi binafsi naona
serikakali ya wilaya ya temeke imeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa mfano
ukiangalia katika barabara hii imejaa maji mpaka hatuwezi kufanya biashara”
alisema ali
Aidha Ali aliongeza kuwa kero zao wameziwasilisha kwenye
serikali ya mtaa huo lakini bado tatizo hilo la muda mrefu halijatatuliwa
“Tumekuwa tukipeleka malalamiko yetu mara kwa mara katika serikali ya mtaa wetu
lakini lakushangaza hatuoni mabadiliko mpaka tumechoka “ Alisistiza Ali.
Kwa upande wake mmoja wa madereva wanaotumia barabara hiyo
Mohammed Bakari ameeleza maskitiko yake juu ya changamototo wanazokumbana nazo
kwenye sekta ya uchukuzi hasa msimu wa mvua “Binafsi naskitika sana na hali ya
barabara zetu gari zinakwama inatubidi tuzunguke mzunguko mrefu sasa
inatupotezea maesabu” alisema Bakari
Mkwelitz BLOG ilifanya juhudi za kumsaka mkuu wa wilaya
ya temeke ili kulidadavua suala hilo lakini juhudi zetu hazikufua dafu.
Malalamishi ya wakaazi hao yamekuja siku chache tu baada ya
mvua kali iliyoshuhudiwa mapema wiki hii katika jiji la Dar es salaam na
vitongoji vyake iliyodumu kwa takriban siku nzima na kuleta athari kwa baadhi
ya maeneo jijini humo.
Tatizo la miundombinu mibovu hususan ya barabara limekuwa tatizo sugu nchini huku
kidole cha lawama kikitupiwa serikali za wilaya na mikoa kwakulifumbia macho
swala hilo.
No comments:
Post a Comment