MECHI za mwisho za Makundi ya UEFA EUROPA LIGI zitafanyika Alhamisi na Timu 22 tayari zimefuzu kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 32 zikibakisha Nafasi 11 zinazogombewa na Timu 22.
Timu 24 ambazo zinaingia Raundi ya Mtoano ya Timu 32 zinatoka Makundi ya EUROPA LIGI na 8 kutoka UEFA CHAMPIONZ LIGI ana hizo ni zile Timu zinazomaliza Nafasi ya 3 ya Makundi hayo na ni moja tu, Borussia Mönchengladbach, ambayo tayari imetua huko na nyingine 7 zitapata uhakika baada ya Mechi za Jumanne na Jumatano.
TIMU 22 ZILIZOFUZU:
Washindi wa Makundi: Ajax, Roma, Schalke, Shakhtar Donetsk, Sparta Praha, Zenit
Wengine waliopita: Anderlecht, APOEL, Athletic, Genk, Krasnodar, Olympiacos, Saint-Étienne
Wanaoweza kusonga Alhamisi: Astra Giurgiu, Austria Wien, AZ Alkmaar, Braga, Celta Vigo, Dundalk, Fenerbahçe, Feyenoord, Fiorentina, Gent, Hapoel Beer-Sheva, Maccabi Tel-Aviv, Manchester United, Osmanlıspor, PAOK, Qarabağ, Slovan Liberec, Southampton, Standard Liège, Steaua Bucureşti , Villarreal, Zürich
Nje: Astana, Gabala, Internazionale Milan, Konyaspor, Mainz, Nice, Panathinaikos, Rapid Wien, Salzburg, Sassuolo, Viktoria Plzeň, Young Boys, Zorya Luhansk
8 kutoka UEFA CHAMPIONZ LIGI:
Ni 8 ikiwa pamoja na Borussia Mönchengladbach ambayo tayari ina uhakika kucheza EUROPA LIGI.
KUNDI A: Feyenoord (Pointi 7) v Fenerbahçe (10), Zorya Luhansk (2) v Manchester United (9)
-Manchester United watafuzu kwa Sare bila kujali matokeo mengine.
-Fenerbahçe, walioshinda 1-0 katika Mechi ya Kwanza, watasonga kwa Sare.
Zorya wako nje.
KUNDI B: APOEL (9, Wamesonga) v Olympiacos (8, Wamesonga), Young Boys (5) v Astana (5)
APOEL wamesonga na watatwaa ushindi wa Kundi kwa Sare.
Olympiacos pia wamefuzu.
Young Boys na Astana wako nje.
KUNDI C: Anderlecht (11, Wamesonga) v St-Étienne (9, Wamesonga), Mainz (6) v Gabala (0)
Anderlecht wamesonga na watatwaa ushindi wa Kundi kwa Sare.
St-Étienne pia wamesonga na watatwaa ushindi wa Kundi kwa ushindi.
Mainz na Gabala wako nje
KUNDI D: AZ (5) v Zenit (15, Wamesonga), Maccabi Tel-Aviv (4) v Dundalk (4)
Zenit wamesonga na kutwaa ushindi wa Kundi.
AZ watasonga wakishinda ama wakitoka Sare ili mradi Gemu nyingine iwe Sare au wakifungwa ikiwa Gemu nyingine ni 0-0.
Dundalk watasonga wakishinda na AZ wasiposhinda au wakitoka Sare ya Magoli wakati AZ wanafungwa.
Maccabi watasonga wakishinda ikiwa AZ hawashindi.
KUNDI E: Astra (7) v Roma (11, Wamesonga), Viktoria Plzeň (3) v Austria Wien (5)
Roma wamesonga na kutwaa ushindi wa Kundi.
Astra watasonga wakishinda au Austria wasiposhinda.
Plzeň wako nje.
KUNDI F: Rapid Wien (5) v Athletic Club (9, Wamesonga), Sassuolo (5) v Genk (9, Wamesonga)
Athletic na Genk wamefuzu.
Rapid na Sassuolo nje.
KUNDI G: Standard (6) v Ajax (13, Wamesonga), Panathinaikos (1) v Celta Vigo (6)
Ajax wamesonga na kutwaa ushindi wa Kundi.
Ikiwa Celta Vigo na Standard Liege, wenye Rekodi zinazofanana, watamaliza wakiwa sawasawa basi Vipengele vingine vya Sheria vitatumika kuamua nani anaungana na Ajax kusonga.
Panathinaikos wako nje.
KUNDI H: Braga (6) v Shakhtar Donetsk (15, Wamesonga), Konyaspior (1) v Gent (5)
Shakhtar wamesonga na kutwaa ushindi wa Kundi.
Braga watasonga kwa ushindi ikiwa watashinda ikiwa Gent fail watashindwa kushinda.
Gent watasonga wakishinda ikiwa Braga hawashindi.
Konyaspor wako nje.
KUNDI I: Salzburg (4) v Schalke (15, through), Nice (3) v Krasnodar (7)
Schalke wamesonga na kutwaa ushindi wa Kundi.
Krasnodar pia wamefuzu.
Salzburg na Nice wako nje.
KUNDI J: QarabaÄŸ (7) v Fiorentina (10), PAOK (7) v Slovan Liberec (4)
Fiorentina wana nafasi kubwa ya kufuzu labda wafungwe na PAOK washinde na hilo litaamuliwa kwa Mechi ya Fiorentina na QarabaÄŸ kwenye Magoli yatakayofungwa.
Qarabag watasonga wakishinda au Sare ikiwa PAOK hawashindi.
Liberec watafuzu wakishinda na QarabaÄŸ wakifungwa.
KUNDI K: Southampton (7) v Hapoel Beer-Sheva (7), Internazionale Milano (3) v Sparta Praha (12)
Sparta wamesonga na kutwaa ushindi wa Kundi.
Hapoel watafuzu wakishinda au kupata Sare ya Magoli lakini wakimaliza 0-0 basi Southampton watasonga.
Inter wako nje.
KUNDI L: Osmanlıspor (7) v Zürich (6), Villarreal (6) v Steaua (6)
Osmanlıspor watasonga wakishinda au Gemu nyingine ikiwa Sare.
Zurich watasonga kwa ushindi.
Villarreal watasonga kwa ushindi au Sare ikiwa Zurich wasiposhinda.
Steaua watasonga kwa ushindi au Sare itakayozidi zile za 0-0 na 1-1 ikiwa Zurich.
No comments:
Post a Comment