KOCHA WA TIMU YA UFARANSA DESCHAMPS AMUONYA PAUL POGBA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Wednesday, December 7

KOCHA WA TIMU YA UFARANSA DESCHAMPS AMUONYA PAUL POGBA

Image result for Didier Deschamps.
Paul Pogba ametakiwa kuweka maslahi ya Timu mbele ili awe na mafanikio akiwa na Manchester United badala ya kutaka kuonyesha uwezo wake binafsi kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Nchi yake France Didier Deschamps.
Mwanzoni mwa Msimu Man United ililipa Dau la Rekodi ya Dunia, Pauni Milioni 89, kumnunua Pogba kutoka Juventus ya Italy lakini mchango wake umekuwa duni na hata Meneja wa Klabu yake, Jose Mourinho, amekiri Kijana huyo anahitaji muda zaidi ili kujiweka sawa kuchezea EPL, Ligi Kuu England, baada ya kuwa Serie A na Juve kwa Miaka Minne.
Meneja wa France Didier Deschamps ametoboa Pogba anajitihidi sana ili kuwanyamazisha wapondaji ambao milele hataweza kuwabadili mawazo.
Deschamps amesema: “Hata akifanya vizuri, kwa wapondaji hao si vyema. Sasa hilo linaweza kumfanya ajaribu vitu vya ajabu ambavyo havisaidii Timu!”
Aliongeza: “Ana uwezo wa kufanya vitu vingi ambavyo wengi hawawezi lakini kitu bora ni kile kizuri kwa Timu!”
Vile vile, Deschamps amekiri Pogba hataweza kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani au ile ya Ballons d'Or.
Deschamps ameeleza: “Yeye ni Kiungo. Washindi wa Ballons d'Or ni Mastraika au Namba 10 ikitokezea. Wao ndo Wafungaji Mabao. Paul? Anafunga lakini hatafunga Bao 3 kila Gemu!”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here