JONAS MKUDE AWEKA WAZI KUHUSU KUJIUNGA NA YANGA SC,HABARI KAMILI HAPA NA MKWELITZ BLOG - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, December 8

JONAS MKUDE AWEKA WAZI KUHUSU KUJIUNGA NA YANGA SC,HABARI KAMILI HAPA NA MKWELITZ BLOG

Image result for jonas mkude wa simba
Kumekua na tetesi za mchezaji na nahodha wa Simba Jonas Mkude kwamba anataka kujiunga na club ya Yanga akitokea Simba.
Tetesi hizi zimepamba moto baada ya mchezaji huyo kushindwa kusafiri na timu kwenda Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili. Akiongea na Sport Xtra Mkude alisema hivi,“Nawezaje kwenda Yanga wakati nina mkataba na Simba, haya ni maneno tu kila mtu anazungumza yake. Mimi ndio mhusika na nataka wajue mimi ni mchezaji halali wa Simba na bado nina mkataba na Simba. 
Hayo maneno yataendelea tu lakini mimi kama mhusika nasema kwamba bado nina mapenzi na Simba na ndio maana bado nipo kwenye mkataba nayo. Maisha yapo hivi, sehemu ambayo ina maslahi na wewe ndipo unapobakia, sina maana sehemu nyingine haiwezi kuwa na maslahi na mimi hapana. Kwa sasa mimi maslahi yangu yapo Simba”
Mkude aliulizwa kuhusu yeye kutaka kusajiliwa na Yanga licha ya kuwa na mkataba alisema hivi,“Siwezi kuzungumzia kujiunga na Yanga wakati nipo Simba. Mimi ni mchezaji wa Simba ndani ya mkataba, swala la kujiunga na Yanga sitakiwi kuzungumzia sasa hivi. Mimi ni mchezaji halali wa Simba”.
Akaulizwa tena kwamba inasemekana anamkwepa kiongozi mmoja wa Simba kwenye swala la kuongeza mkataba, Mkude akajibu,“Kiongozi gani alinitafuta mimi nikamkwepa. Nawezaje kumkwepa kiongozi wangu. Simu gani nilipigiwa sikupokea, hayo yote ni maneno tu yanasambaa”.
Kuhusu picha inayosambaa Mkude alijibu,“Hiyo picha ni ya zamani sana mwaka 2014 nashangaa inasambaa sasa hivi. Naomba nimalize mimi nipo Simba ndani ya mkataba siwezi kufanya chochote zaidi ya kucheza Simba kwa sasa”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here