MANCHESTER UNITED YAPITA KIBABE HATUA YA MTOANO EUROPA LEAGUA,MATOKEO NA HABARI KAMILI HAPA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Friday, December 9

MANCHESTER UNITED YAPITA KIBABE HATUA YA MTOANO EUROPA LEAGUA,MATOKEO NA HABARI KAMILI HAPA

Image result for manchester united
Manchester United wakihitaji Pointi 1 ili kufuzu huko Chornomorets Stadium, Odessa, Ukraine, Uwanja ambao uliganda kwa baridi kama mawe na nusura iahirishwe, Manchester United wamevuna Pointi 3 walipoichapaZorya Luhansk 2-0 kwenye Mechi ya Kundi A na kufuzu Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI.
Image result for manchester united
Pamoja na Man United, Fenerbahce nao wanatinga Raundi ya Mtoano ya Timu 32 baada kuifunga Feyenoord huko Rotterdam Bao 1-0.
Jose Mourinho, Meneja wa Man United, alibadili Wachezaji Watano toka kile Kikosi kilichoanza Mechi ya Jumapili ya EPL, Ligi Kuu England, walipotoka Sare 1-1 na Everton.
Hadi Mapumziko, Mechi hii ilikuwa 0-0.
Kipindi cha Pili, Dakika ya 3 tu tangu kuanza, Henrikh Mkhitaryan alipasiwa pasi safi na Marcos Rojo na kuchanja mbuga akiwatambuka Mabeki wa Zorya na kufunga Bao lake la kwanza kwa Man United.
Dakika ya 88, Zlatan Ibrahimovic aliipa Man United Bao la Pili.
Image result for manchester united
Man United watajua Wapinzani wao wa Raundi ya Mtoano ya Timu 32 hapo Jumatatu itakapofanyika Droo ya Raundi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here