MAHAKAMA ya Michzo ya
Kimataifa-CAS, imetupilia mbali rufani ya rais wa zamani wa Shirikisho la Soka
Duniani-FIFA Sepp Blatter aliyepinga kufungiwa kujishughulisha na shughuli za
soka kwa miaka sita.
Blatter mwenye umri wa miaka 80, alifungiwa kufuatia kukiuka
maadili ya shirikisho hilo aliloliongoza kwa miaka 17, kufuatia kashfa za
ufisadi zilizoibuka mwaka jana.
Blatter alikutwa na hatia ya kufanya malipo
yasiyo halali ya paundi milioni 1.3 kwenda kwa rais wa zamani wa Shirikisho la
Soka la Ulaya-UEFA Michel Platini ambapo wote walikanusha kufanya jambo lolote
baya.
Mara baada ya uamuzi huo wa CAS, Blatter amesema hatakata rufani na
amekubaliana na uamuzi huo.
Blatter aliongeza kuwa kwa uzoefu wake wa miaka 41
katika soka kikubwa alichojifunza ni kwamba unaweza kushinda katika mechi
lakini pia unaweza kushindwa.
No comments:
Post a Comment