Uongozi wa klabu ya Simba umejipanga kuleta kiungo mpya mkabaji kuchukua nafasi ya nahodha wake Jonas Mkude.
Simba iko katika mazungumzo na mmoja wa wakala katika nchi za Afrika Magharibi na inaelezwa itamleta kiungo huyo ndani ya siku mbili.
Uamuzi huo wa Simba, umefikiwa baada ya kuona Mkude akiwazungusha.
“Zaidi anazima simu au anafanya makusudi kutotuona. Jiulize, mtu anayetaka mfikie mwafaka wa jambo, vipi atajificha. Hii ni ajabu kabisa,” kilieleza chanzo kutoka Simba.
“Mtu kama Mkude ambaye tumemlea, angalau kama ana jambo, basi aseme. Akijificha maana yake nini, dharau? Au Simba haiwezi kupata mchezaji kama yeye? Acha tuhangaike na itawezekana tu.”
No comments:
Post a Comment