Kiongozi mmoja wa Simba, amesema hawana nia mbaya au ugomvi na
nahodha wao, Jonas Mkude.
Lakini ulichoshwa na namns alivyoamua kuchukua uamuzi wa kuwakimbia kama sehemu
ya kuwakomoa.
Tayari Simba iko katika mazungumzo ya mwisho ya kumsajili kiungo kinda aitwaye
James Kotei raia wa Ghana.
Taarifa za awali, zilieleza Mkude alihitaji Sh milioni 80 wakati Simba ilianzia
Sh milioni 50, mwisho ikakomea kwenye milioni 60 na yeye akaona hazitoshi,
akazima simu.
Hata hivyo, awali pia Mkude alihojiwa na kusema aliamua kuzima simu baada ya
baadhi ya ndugu kuanza kumsumbua baada ya kuzikia alishapewa fedha za usajili
baada ya kiongozi mmoja wa Simba kusema wamemalizana, jambo ambalo halikuwa
sahihi.
No comments:
Post a Comment