BAKWATA yafafanua sikukuu ya Idd el-Fitr - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Saturday, June 24

BAKWATA yafafanua sikukuu ya Idd el-Fitr


Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakary Zuberi Ally

Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir Bin Ally amesema Baraza kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA linaendelea kufuatilia kuandama kwa mwezi na kwamba litatoa taarifa kamili juu ya siku ya kufanyika kwa sikukuu ya Idd el-Fitr kama ni kesho au kesho kutwa.

Mufti, Aboubakar Zubeir Bin Ally ametoa kauli hiyo jana jioni kufuatia taarifa kupitia mitandao ya kijamii zilizozagaa na kusema kuwa sikukuu ya Idd el-Fitr itakuwa siku ya Jumatatu.

Mufti amesema hilo halijatangazwa na kufafanua kwamba Mufti ndiye mwenye mamlaka ya kutangaza baada ya kushauriana na kamati ya mwezi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here