Makaburi 10 ya pamoja yagunduliwa DRC - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Tuesday, June 27

Makaburi 10 ya pamoja yagunduliwa DRC


Waliozikwa wanasemekana kuuawa na waasi

Mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inasema kwamba imepata zaidi ya makaburi kumi ya pamoja katika mkoa wa Kasai, mahali ambapo vikosi vya serikali na makundi ya waasi yametuhumiwa kwa mauaji ya raia.

Mwendesha mastaka wa kijeshi Generali Joseph Ponde amesema anaamini mauaji hayo yamefanywa na sehemu waasi wa Kamuina Nsapu ambao wamekuwa wakipiga vita majeshi ya serikali.

Mnamo wiki iliyopita Umoja wa Mataifa ulielezea hofu yake juu ya mauaji yanayoendelea kila uchao katika mkoa huo, ambapo takriban watu elfu mbili waliangamizwa katika kipindi cha miezi mitatu.

Umoja huo aidha ulinyooshea kidole jeshi la taifa la Kongo kwa kutekeleza uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu.

Hata hivyo jopo maalum la uchunguzi wa mauaji hayo iliamua kwamba hakuna uhalifu wowote wa kivitu uliyotekelezwa na kwamba hakuna mapigano yaliyotangazwa rasmi mkoani Kasai.

Inadaiwa baadhi ya wanajeshi hao walinaswa katika kanda ya video wakiwapiga risasi raia ambao hawakuwa na silaha.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here