Mbunge auwasha moto Bungeni - MKWELITZ BLOG

.

demo-image-Recovered

.

Capture

Tuesday, June 6

Mbunge auwasha moto Bungeni


8884-Joseph+Kakunda
Dodoma. Mbunge wa Sikonge (CCM), Joseph Kakunda amewasha moto bungeni baada ya kukerwa na upembuzi yakinifu wa barabara ya Ipole hadi Rungwa mkoani Tabora kuchukua miaka 43 tangu Serikali ianze kutoa majibu kuhusu ujenzi wa barabara hiyo.

 Katika swali la msingi mbunge huyo ameuliza sababu ya  upembuzi yakinifu kwa ajili ya kuijenga barabara hiyo ambayo ni sehemu ya barabara kuu inayounganisha Mkoa wa Tabora na Mbeya, kuchukua miaka mingi.

 “Katika mwaka wa fedha 2016/2017 barabara hiyo ilitengewa Sh350 milioni kwa ajili ya upembuzi yakinifu na bado usanifu wa kina unahitajika,”mbunge huyo amehoji ni lini barabara hiyo itajengwa katika kiwango cha lami.

“Upembuzi yakinifu ulianza mwaka 1974 sasa ni miaka 43 haijakamilika.Lini Serikali itaijenga barabara hii katika kiwango cha lami? Amehoji na kuongeza;

 “Kama Serikali haitaji muda maalumu wa ujenzi wa barabara hii je haiashirii kuwa haina mpango wa kuiweka katika mpango maalum wakuijenga barabara hii katika kiwango cha lami?

 Akijibu maswali hayo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Mhandisi Edwin Ngonyani amesema kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ikiwa ni pamoja na uandaaji wa nyaraka za zabuni kwa barabara hiyo yenye urefu wa Km 172 inaendelea.

“Katika mwaka wa fedha 2016/17 jumla ya Sh1.2 bilioni zimetengwa na katika mwaka wa fedha 2017/18 zimetengwa Sh435 milioni kwa ajili ya kukamilisha kazi hiyo,”amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad