Mchezaji wa Bayern Munich atiwa mbaroni kwa kumpiga mpenzi wake - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Wednesday, June 28

Mchezaji wa Bayern Munich atiwa mbaroni kwa kumpiga mpenzi wake


Ujerumani. Mshambuliaji wa Bayern Munich, Kingsley Coman anashikiliwa na polisi kutokana na kumfanyia vurugu mpenzi wake wa zamani.

Mshambuliaji huyo anadaiwa kumfanyia vurugu mpenzi wake, Seine et Marne baada ya kumfuata nyumbani kwake.

Ofisi ya makosa ya upelelezi nchini Ufaransa ilithibitisha mchezaji huyo mwenye miaka 21 alikamatwa na polisi mjini Chessy ikiwa na umbali wa miles 25 kutoka jijini Paris alikomfuata mpenzi wake na kumfanyia vurugu.

Chanzo cha ugomvu huo inaelezwa ni kutokana na kutoelewana kuhusu fedha za matangazo ambazo wawili hao waliwahi kuingia mkataba na kampuni moja nchini humo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here