MWANAMUZIKI anayetamba na Ngoma ya Manuari, Kassimu Mganga amesema moja kati ya ndoto zake kipindi anaanza muziki ilikuwa ni kuwa mwanamuziki mkubwa wa Hip Hop.
Akizungumza na Risasi Vibes, Kassimu alisema tangu akiwa mkoani Tanga alikuwa ni mpenzi mkubwa wa Muziki wa Hip Hop na ndoto yake ilikuwa ni kuwa mwanamuziki mashuhuri wa miondoko hiyo hata hivyo mawazo yake yalibadilika baada ya kutimkia visiwani Zanzibar.
“Nikiwa Tanga nilitamani siku moja niwe mwanamuziki mkubwa wa Hip Hop kama Prof Jay, lakini ndoto zangu zilipotea baaada ya kwenda Zanzibar ambako waandaaji wa muziki walinishauri nibadili mtindo wa uimbaji, ndipo nilipotoa kibao kiitwacho ‘Haiwezekani’ nikajiona naweza kuimba kuliko muziki wa kufokafoka,” alisema Kassimu.
No comments:
Post a Comment