Rick Ross afuta picha za Diamond - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Saturday, January 27

Rick Ross afuta picha za Diamond


Staa wa muziki kutokea nchini Marekani Rick Ross  January 26,2018 alichukua headlines katika mitandao ya kijamii baada ya kujulikana kafuta picha zote za Diamond Platnumz katika ukurasa wake wa Instagram.

 Rick Ross amewahi kumpost mara mbiliDiamond Platnumz kupitia ukurasa wake wa instagram, post zote zikihusiana na ishu ya ubalozi wa kinywaji cha Belaire mwezi September 2017.

 Maswali yamezidi kuwa mengi kutoka kwa mashabiki baada ya Rick Ross kutofuta picha za kinywaji cha Belaire na kuacha picha yaHuddah Monroe ambaye pia ni balozi wa kinywaji hicho kutokea nchini Kenya lakini post za Diamond pekee ndio amefuta.

Nini kinaendelea kati ya Diamond na Rick Ross? ikumbukwe tu Rick Ross na Diamond Platnumz wameshafanya kazi pamoja katika wimbo wa Waka Waka ambao ulifanyika nchini Marekani.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here