Singida: Baada ya Juventus kupokea kipigo kutoka kwa Madrid, kumepelekea shabiki kufariki dunia - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Tuesday, June 6

Singida: Baada ya Juventus kupokea kipigo kutoka kwa Madrid, kumepelekea shabiki kufariki dunia


Shabiki wa Juventus alipoteza maisha baada ya timu yake kufungwa 4-1 na Real Madrid Juni, 2017 kwenye mchezo wa fainali ya UEFA Champions League na kupoteza ubingwa wa taji hilo kubwa barani Ulaya kwa ngazi ya vilabu.

Aloyce Florian Mwimbwa mkazi wa Itigi, Manyoni, Singida alipoteza uhai baada ya kushuhudia timu anayoishabikia ikishindwa kupata matokeo ya ushindi mbele ya Madrid ambao wamelitetea taji hilo kwa mara ya kwanza katika historia.

Mdogo wa marehemu amethibitisha kaka yake kufariki kutokana na matokeo ya mchezo huo na kutaarifu kwamba, marehemu alikuwa anasumbuliwa na tatizo la pressure kushuka.

“Tukio lilitokea siku ya mechi ya majuzi kati ya Juve na Real Madrid, kaka yangu alikuwa ni mpenzi sana wa Juve. Kaka alikuwa na tatizo la pressure ya kushuka, sasa baada ya Juve kufungwa katika utani wa hapa na pale, pressure ikashuka basi ikawa ndio tatizo la yeye kupoteza maisha,” amesema Sabinu Florian wakati akizungumza na Edgar Kibwana kwenye kipindi cha Sports Extra ndani ya Clouds FM.

“Kabla ya mchezo hali yake ilikuwa ni nzuri na alikuwa na marafiki zake nyumbani kwake wanaangalia mpira, alikuwa haumwi chochote zaidi ya hilo tatizo la pressure. Kwa hiyo baada ua Juve kufungwa hilo tatizo likaja ghafla na akapoteza maisha.”

“Marehemu amekuwa shabiki wa Juventus kwa zaidi ya miaka nane au 10.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here