Naibu kamishna wa polisi mkoa wa Kigoma Fredinand Mtui amesema tukio la ajali limetokea majira ya saa kumi na mbili na nusu jioni ambapo gari lenye namba za usajiri T185 AGP Scania mali ya kampuni ya NBS iliacha njia na kupinduka na kusababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi nane.
Mtui amesema chanzo cha ajali hiyo ni mara baada ya dereva kushindwa kulimudu gari wakati wa kukata kona na hivyo gari hilo liliacha njia na kupinduka ambapo dereva alikimbia.
Wakati huo huo Mtui ametoa taarifa ya mkazi mmoja kufa maji wakati akiogelea katika Bwawa la Katosho lililopo kata ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji.
No comments:
Post a Comment