Amuua mjombaye kisa, gunia moja la alizeti - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Sunday, July 2

Amuua mjombaye kisa, gunia moja la alizeti


Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Benjamin Zakaria (22), anadaiwa kumuua mjomba wake aliyefahamika kwa jina la Adam Joseph (30) kwa madai kuwa alikuwa akimdai gunia moja la alizeti.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana (Jumamosi) baada ya Zakaria kumfuata mjomba wake huyo kwenye kilabu cha pombe na kuanza kumdai gunia hilo la alizeti.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ninga, wilayani Kalambo mkoani Rukwa, Yohana Kawea alisema baada ya watu hao kubishana kwa muda, ndipo Zakaria alichomoa kisu na kumchoma nacho Joseph ambaye alifariki dunia papo hapo.

Alidai kuwa baada ya kumuua, alitokomea na uongozi wa kijiji baada ya kupata taarifa za mauaji hayo, uilipeleka taarifa polisi kwa hatua zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here