Taarifa hiyo imetolewa na wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo siku ya Jumapili.
Mamlaka nchini Misri inaamini kwamba kundi la Hasm ni kundi linalounga mkono na kushirikiana na kundi la Muslim Brotherhood nchini humo.
Kundi la Muslim Brotherhood hata hivyo limekataa madai hayo ya kuhusika na Hasm hasa kwa kuwa mara nyingi husababisha ghasia na vurugu.
Mnamo mwaka 2013 ghasia zilizuka Misri baada ya jeshi nchini humo kupindua serikali ya demokrasia chini ya uongozi wa rais wa zamani Mohammed Morsi.



No comments:
Post a Comment