Mlipuko wasababisha kifo cha mtoto na majeruhi 17 kambini Somalia - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Sunday, July 23

Mlipuko wasababisha kifo cha mtoto na majeruhi 17 kambini Somalia


Mtoto wa kike ameripotiwa kufariki na watu wengine 17 kujeruhiwa baada ya kombora kulipuka  katika kambi ya IDP nchini Somalia siku ya Jumamosi.

Kwa mujibu  wa habari,mamlaka imesema kuwa watoto walikuwa wakichezea kombora hilo  wakidhani kuwa ni mpira wa kuchezea wakati kombora hilo likÅŸlipuka.

Ripoti zinaonyesha kuwa bomu hilo aina ya Grenade liliokotwa na mtoto nje ya kambi na kuletwa ndani kwa ajili ya kuchezea.

Majeraha wote mpaka sasa wamefikishwa hospitalini.

Kambi ya IDP ipo katika kijiji cha Ari Adeye kaskazini mwa Lasanod.

Mpaka hivi sasa haijajulikana bado ni nani anahusika na kutupa bomu hilo ardhini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here