Umoja wa Maifa wapinga Kufungiwa kwa Al-Jazeera - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Saturday, July 1

Umoja wa Maifa wapinga Kufungiwa kwa Al-Jazeera





Umoja wa Mataifa umesema kutaka kufungwa kwa kituo cha matangazo cha Al-Jazeera chenye makao yake nchini Qatar ni shambulio lisilokubalika kwa uhuru wa kujieleza na kutowa maoni.

Kufungwa kwa kituo hicho ni mojawapo ya madai 13 yaliowekewa serikali ya Qatar na Saudi Arabia na washirika wake kama adhabu ili nchi hizo ziiondelee vikwazo ilioiwekea nchi hiyo kwa takriban mwezi mmoja sasa.

Nchi hizo nne zimeipa Qatar siku 10 kutekeleza masharti hayo ambayo muda wake wa mwisho unamalizika Julai nne.

Mkuu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Raa'd Al Hussein ana wasi wasi mkubwa sana na madai kwamba Qatar ikifunge kituo cha Al-Jazeera na vyombo vyengine vya habari vinavyohusiana navyo hayo yamebainishwa na msemaji wake Ruper Colvile alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Ijumaa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here