Watu Sita wanashikiliwa kwa kuchoma moto nyumba 3 - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Monday, July 24

Watu Sita wanashikiliwa kwa kuchoma moto nyumba 3


Jeshi la polisi mkoani Pwani, linawashikilia watu sita kutokana na tukio la kuchoma moto nyumba za watu watatu tofauti na kusababisha hasara ikiwepo kuteketeza pikipiki mbili zenye thamani ya milioni 3.9

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, (ACP) Jonathan Shanna ,amewataja watu hao kuwa ni pamoja na Omary Athumani, Abdallah Shomari, Seif Shomari, Uzalimala Selasela,Salum Shomari na Jumanne Omary wote wakazi wa Vikumburu .

Aidha RPC Pwani amesema watu wote hao wanadaiwa kuchoma nyumba moto ya Bwana Joseph Simbayi, Rebeka Yona na Selina Simon .

Hata hivyo ,kamanda Shana ameeleza watuhumiwa hao pia waliingia kwenye mazizi na kukatakata mifugo ambayo walichukua nyama na vichwa ambapo utumbo waliuacha licha ya idadi ya mifugo hiyo kutofahamika.

Watuhumiwa wote hao wanashikiliwa na jeshi la polisi na pindi uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here