Mkuu wa Wilaya ya Igunga, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, John Mwaipopo aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Meckson Manase, mwanafunzi kutoka Mtaa wa Masanga na Fanueli Charles, mvuvi wa samaki anayeishi Mtaa wa Fisi.
Alisema mwanafunzi aliyefariki dunia pamoja na mvuvi huyo pia, walikuwa wakibeba watu kwa kuwavusha kutoka eneo moja kwenda lingine.
Mwaipopo aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi kwa mtu atakayebainika akiendesha shughuli za uvuvi haramu katika bwawa hilo.
Mtendaji wa Kata ya Igunga, Robert Mwagara alisema wote wawili walizama maji Juni 28 majira ya jioni na miili yao ilipatikana Juni 29 saa 11 alfajiri.
Aliwataka wazazi kutowaruhusu watoto wao kujihusisha na shughuli za uvuvi na kwamba mzazi yeyote atakaye kaidi hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Christopher Edward na Lusia Lazaro ni wakazi wa Igunga kwa nyakati tofauti waliiomba Serikali kuwakamata wavuvi wote wanaoendesha shughuli za uvuvi haramu kwenye bwawa hilo.
No comments:
Post a Comment