Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Brazil alivunja rekodi ya uhamisho kwa kitita cha £200m kwa timu hiyo ya Ufaransa mnamo mwezi Agosti baada ya kununua kandarasi yake katia klabu ya Barcelona .
Barcelona sasa inamtaka kurudisha marupurupu aliyopewa baada ya kutia saini kandarasi mpya ya miaka mitano miezi tisa pekee kabla ya kulazimisha uhamisho huo.
''Klabu inataka mchezaji huyo kurudisha marupurupu aliyolipwa kwa kuwa hakumaliza kandarasi yake'', ilisema taarifa.
Mbali na Yuro milioni 8.5 za marupurupu, klabu hiyo pia inataka kulipwa asilimia 10 ya fedha hizo kwa kuchelewa kulipwa.
Taarifa hiyo iliendelea: Barcelona pia inaitaka PSG kuchukua jukumu la kulipa fedha hizo iwapo mchezaji huyo atashindwa kulipa.
Kufuatia uhamisho huo Barcelona ilitangza kuwa inazuilia Yuro milioni 26 za marupurupu ambazo mchezaji huyo alifaa kulipwa.
No comments:
Post a Comment