Beki Mghana akaribia kutua Ligi Kuu England - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Tuesday, August 15

Beki Mghana akaribia kutua Ligi Kuu England


KOCHA wa Barnsley, Paul Heckingbottom hawezi kumtumia Andy Yiadom anayetakiwa na Huddersfield Town kwa sababu yuko njia panda.

Beki huyo Mghana mwenye umri wa miaka 25, aliyewasili kutoka timu ya Ligi Daraja la Pili, Barnet mwezi Mei mwaka 2016, aliachwa kwenye kikosi kilichofungwa nyumbani na Ipswich Jumamosi baada ya kuanzishwa katika mechi mbili zilizotanguli.

Heckingbottom amesema mazungumzo na timu hiyo mpya ya Ligi Kuu yam England yanaendelea. "Machoni mwangu, simuoni Yids hadi nitakapoambiwa tofauti,"amesema.

"Haikuwa sahihi kwangu kumjumuisha Yids katika mchezo wa Jumamosi na ikiwa itabaki kama ilivyo, hatacheza na Jumanne pia kwa sababu haitakuwa vizuri kwa wachezaji wengine,".

"Tunajiandaa kwa mchezo wetu na dhahiri Yids yuko njia panda kwa sasa. Hadi itakapojulikana moja na nikaambiwa, simfikirii," amesema.

Heckingbottom amesema mazungumzo juu ya mchezaji huyo aliyecheza mechi 33 za Ligi Daraja la Kwanza, maarufu kama Championship msimu uliopita yanaendelea,.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here