DR Congo: Zaidi ya watu 40 wauwawa kwenye maporomoko ya ardhi - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, August 17

DR Congo: Zaidi ya watu 40 wauwawa kwenye maporomoko ya ardhi


Zaidi ya watu 40 wameuawa kwenye janga la maporomoko ya ardhi kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.

Wengi wa wale waliouawa ni kutoka kijiji kimoja kinachofanya uvuvi katika kingo za ziwa Albert.

Mvua kubwa imesababisha sehemu za mlima ulio karibu kuporomoka na kufunika kijiji hicho.

Watu wengine kadhaa walifariki wakitafuta dhahabu kwenye migodi ya zamani.

Kumekuwa na majanga mabaya ya maporomo ya ardhi mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo miaka ya hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here