Kocha Ancelotti akatazwa kuvuta sigara - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Saturday, August 19

Kocha Ancelotti akatazwa kuvuta sigara


Kocha wa FC Bayern Munich ya Ujerumani Carlo Ancelotti ni mmoja kati ya makocha ambao wanavuta sigara, Ancelotti amekuwa na utamaduni wa kupenda kuvuta sigara akiwa mazoezini, kitendo ambacho akimfurahishi mkurugenzi wa michezo wa Bayern.

Leo August 18 Carlo Ancelotti ameambiwa na mkurugenzi wa michezo wa FC Bayern Hasan Salihamidzic kuacha kuvuta sigara akiwa maeneo ya club ya timu hiyo na mazoezini, maamuzi ambayo Ancelotti ameyakubali na ataachana na utamaduni huo.

“Nimemuomba Ancelotti asiwe anavuta sigara akiwa club kiukuweli amekubali, Ancelotti ni professional” - Hasan Salihamidzic

Kocha Carlo Ancelotti mwenye umri wa miaka 58 amewahi kukiri kuwa alianza kuvuta sigara toka akiwa na umri wa miaka 25 “Nilikuwa sivuti sigara katika maisha yangu sema nilijaribu siku moja, kwa sasa huwa navuta nikiwa nime-relax, baada ya dinner au ninapokuwa naangalia movie” - Carlo Ancelotti

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here