Liverpool wakataa ofa ya tatu kutoka Barcelona ili wauziwe Coutinho - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Saturday, August 19

Liverpool wakataa ofa ya tatu kutoka Barcelona ili wauziwe Coutinho


Baada ya mshambuliaji wa Brazil Neymar kuvunja mkataba na FC Barcelona na kujiunga na club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa kwa ada ya uhamisho ya dunia ya pound milioni 199, Barcelona wameelekeza nguvu zao kwa mbrazil mwingine Philippe Coutinho wa Liverpool.

Barcelona ambao kwa sasa wanahangahika kupata mbadala wa Neymar ambaye ndio wanaona kuwa Coutinho atafaa, wamekataliwa ofa ya tatu ya pound milioni 113  ambayo inaweza kufikia hadi pound milioni 118 kwa Liverpool ili wakubali kumuachia nyota huyo ajiunge na Barcelona.

Coutinho ni moja kati ya wachezaji wa Liverpool waliyoisaidia timu hiyo kumaliza nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu msimu 2016/2017 na kujihakikishia nafasi ya kucheza UEFA Champions League, Coutinho katika msimu wa 2016/2017 wa EPL ameifungia Liverpool magoli 13 na kutoa assist saba katika michezo 31 aliyocheza.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here