LWANDAMINA.
Yanga ipo Pemba, Zanzibar ikiendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo inatarajiwa kufanyika kuanzia Agosti 26 mwaka huu.
Akizungumza na gazeti hili jana, Lwandamina alisema kuwa asilimia kubwa ya programu yake ya mazoezi imekamilika na kikosi chake kinasubiri siku na muda wa mechi hiyo ifike.
"Sasa hivi tunafanya mambo madogo madogo, lakini kimsingi kikosi changu kipo tayari kwa mikikimikiki ya Ligi Kuu," alisema Lwandamina.
Aliongeza kuwa siku zilizobakia kabla yakurejea Dar es Salaam kukabiliana na Simba, anaondoa baadhi ya mapungufu aliyoyaona kwenye michezo ya kirafiki ambayo wamecheza hivi karibuni.
Alisema pia mazoezi wanayofanya yanalenga kujiandaa kupambana na timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu Bara na sio Simba peke yake.
"Najua tuna michezo mitatu dhidi ya Simba, hivyo maandalizi yetu si kwa ajili ya mechi hizo dhidi ya Simba peke yake, tumefanya maandalizi kwa ajili ya mechi zetu zote zilizopo mbele yetu kuanzia ile ya ligi pamoja na michuano ya kimataifa," Lwandamina alisema.
Mzambia huyo alisema anafurahi kuona wachezaji wake wanazidi kuwa imara na anaomba nyota wake wasipate majeruhi, ili awe na wigo mpana wa kupanga kikosi anachotaka.
Yanga itashuka uwanjani Jumatano ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa mabao 2-1 katika mchezo wa mwisho walipokutana watani hao wa jadi.
No comments:
Post a Comment